Afya za familia zetu huanza na sisi wenyewe hasa kwenye mwenendo wa vyakula vyetu tunavyo kula majumbani mwetu. Afya ya mwili hujumuisha afya ya meno na hapa ningependa kukushirikisha wewe msomaji katika kile nilicho kuandalia.
Huwa tunajisahau kwamba kuwa meno mazuri ni afya na afya nzuri ya meno hasa huanza na umri mdogo. Watoto wetu wakitunza na kufundishwa kutunza meno yao basi watakuwa na afya nzuri ukubwani. Hivyo basi ni jukumu letu sisi kama wazazi kuwafundisha watoto wetu juu ya afya ya meno ikiwemo kuwapa nafasi ya kutambua umuhimu wa kusafisha meno mara kwa mara ili kuwa na meno imara.
Tunaweza haribu meno yetu ikiwa tutaupa mwili kipaumbele cha kula vitu vyenye sukari nyingi. Pia uwingi wa sukari mwilini unasababisha magonjwa mengi na matabibu huwa wanatusisitiza kula kiwango kidogo cha sukari.
Katika kuendelea kujifunza kuhusu afya na mlo kamili basi nimekuja na tip itusaidie pamoja.
Nini cha kufanya?
1. Download document na print kwa mfumo wa rangi.
2. Soma na pamoja mwanao weka alama ya tabasamu sehemu yenye kiduara kwa kila tunda au bonga apendayo.
3. Itundike sehemu itakapoonekana ili iwe rahisi kwa familia nzima kuona snacks wanazo ruhusiwa kubeba Shuleni.
4. Mjulishe na rafiki yako kuhusu hili.
Note. Comment kuhusu wazo hili na asante kwa kushare na wengine.
Kommentar hinzufügen
Kommentare
Asante kwa kushare. Hii itanisaidia mimi na baba changa. Kwasababu muda mwingine nakosa wazo la cha kuwapa watoto pindi waendapo Shule.
Asante Rehema. Basi endelea kufurahia wazo hili wewe na familia yako.
Mimi nimesha pata yangu. Asante kwa wazo hili linanifaa sana. Nitakupa mrejesho kupitia instagram yako. 🫶🏾💚
Asante sana kitu kizuri